13 Oct 2020 / 227 views
Young akutwa na virusi vya Corona

Klabu ya Inter Milan imethibitisha kuwa kiungo wao, Ashley Young amekutwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona baada ya kufanyiwa vipimo vya ugonjwa huo.

"Ashley Young amekutwa na virusi vya Covid-19 kufuatia vipimo viliyofanywa siku ya  Jumamosi huko Appiano Gentile," ilisema taarifa ya klabu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Watford na Aston Villa Young alijiunga na Inter kutoka Manchester United mnamo Januari mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anakuwa mchezaji wa sita kupipima katika klabu hiyo baada ya viungo Radja Nainggolan na Roberto Gagliardini, beki Milan Skriniar, Alessandro Bastoni na kipa Ionut Radu.

Washindi wa pili wa Serie A Inter Milan watakutana na wapinzani wao wa jiji la AC Milan mnamo Oktoba 17 kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini Italia Seria A.

Mechi hiyo bado ina mashaka na watetezi wawili wa wachezaji wa Milan Leo Duarte na Matteo Gabbia kwa sasa wamejitenga.

Nyota wa Milan kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic alirudi mazoezini Jumapilibaada ya kupimwa na ugonjwa huo mnamo Septemba 24.

AC Milan inashika nafasi ya pili katika Serie A baada ya kushinda michezo yao yote mitatu, na Inter Milan ikiwa ya nne baada ya kushinda mara mbili na sare.